Na George Binagi, Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza kusitishwa shughuli za uchimbaji madini katika machimbo ya Epanko iliyopo eneo la Mahenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kutokana na machimbo hayo kukiuka kanuni na sheria za uendeshaji.
Naibu Waziri Biteko ametoa agizo hilo leo 10 Julai 2018 ametoa agizo hilo kufuatia ripoti ya timu maalumu aliyoiunda mwezi uliopita na Kamishina wa Madini nchini kuonyesha hakuna usimamizi na udhibiti mzuri wa madini ya vito aina ya Spinel, Green-Gernel pamoja na Ruby katika machimbo hayo na hivyo kuikosesha serikali mapato.