Duration 47:44

Zuhura Yunus: Nafahamu Hisia Zitakazoibuliwa na Kitabu Changu

3 712 watched
0
48
Published 14 Nov 2021

Mnamo Novemba 9, 2021, mwandishi wa habari na mtangazaji mashuhuri wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Zuhura Yunus alizindua kitabu chake kiitwacho Biubwa Amour Zahor: Mwanamke Mwanamapinduzi. Kitabu hicho kinachohusu maisha na mchango wa mwanamama huyo wa Kizanzibari katika Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, pia kilizinduliwa Dar es Salaam, mnamo Novemba 13. 2021, katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na wanazuoni, waandishi wa vitabu, wanaharakati na waandishi wa habari. Kufuatia uzinduzi huo, The Chanzo imefanya mahojiano maalum na Zuhura ili kujadili baadhi ya mambo yanayopatikana kwenye kitabu hicho. #TheChanzo

Category

Show more

Comments - 11